UJUMBE WA MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI – MKOA WA PWANI

SEMINA MBALIMBALI Semina mbalimali

Posted by admin on 2026-03-17 11:33:59 |

Share: Facebook | Twitter | Whatsapp | Linkedin Visits: 32


UJUMBE WA MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI – MKOA WA PWANI

Shirika la Equip for Change lilishiriki katika maadhimisho ya International Women's Day yaliyofanyika tarehe 8 Machi 2026 katika Rufiji District. Maadhimisho haya ya kimkoa yaliwakutanisha wadau mbalimbali kutoka taasisi za serikali, mashirika ya kiraia, sekta binafsi pamoja na vikundi vya wanawake ili kuungana na dunia katika kutambua mchango mkubwa wa wanawake katika maendeleo ya jamii.

Maadhimisho ya mwaka huu yalibeba ujumbe rasmi unaosema:

“Accelerate Action for Gender Equality” yaani “Kuharakisha Hatua za Kufikia Usawa wa Kijinsia.”

Kupitia ujumbe huu, jamii ilihimizwa kuongeza juhudi katika:

Kuwawezesha wanawake kiuchumi

Kulinda haki na usalama wa wanawake na watoto wa kike

Kukuza elimu na nafasi za uongozi kwa wanawake

Kupinga ukatili wa kijinsia

Kujenga jamii yenye usawa, haki na heshima kwa wote.

Ushiriki wa wadau mbalimbali katika maadhimisho haya uliendelea kuonesha dhamira ya pamoja ya kutambua na kuenzi mchango wa wanawake katika maendeleo ya familia, jamii na taifa.

Kwa pamoja tunaweza kujenga jamii inayowathamini wanawake na kuwawezesha kufikia uwezo wao kamili kwa maendeleo endelevu ya jamii na taifa. 


Leave a Comment: